Karibuni sana!


fair trafe kaffee, kenia kaffee, ndurutu, chania

 

Jina langu ni Luisa Maria Marijani na nina furaha sana kuwakaribisha wote kwenye duka langu la mtandaoni.

 

Kahawa ni fahari yangu na ni mipango yangu kuwashirikisha kwenye kahawa yenye ubora wa hali ya juu kutoka Afrika Mashariki.

 

 

Uhuru Coffee ilianzishwa kujumuisha fahari zangu mbili kubwa katika maisha yangu: hisia zangu kwenye kinywaji cha kahawa na mapenzi yangu kwa Bara la Afrika na watu wake.

 

 

Nimetunukiwa shahada ya uzamili katika masomo ya historia ya Afrika ( African Studies) kutoka Chuo Kikuu cha Humboldt mji wa Berlin (Ujerumani) na katika masomo yangu nimetumia muda mwingi kuwepo Afrika Mashariki muda mrefu katika kipindi cha miaka sita iliyopita.

Katika muda ambao nilikuwa nchini Tanzania nilipata nafasi ya kutembelea mashamba mbalimbali ya kahawa na kukutana na wakulima kama maeneo ya mkoa wa Kilimanjaro.

Baada ya kuona kazi inayofanywa na wakulima hao na maisha yao kwa ujumla yalinigusa sana. Na nilisema na moyo wangu kwamba nitajishughulisha na biashara ya kahawa baadaye.

 

Mwaka 2012 nilikutana na Muthoni Schneidewind kutoka nchini Kenya ambaye anaishi Ujerumani pamoja na familia yake. Mrs Schneidewind anaendesha shirika lisilo la kiserikali, jina lake ni Kedovo e.V.  Shirika hilo linaingiza kahawa kwa wingi nchini Ujerumani, kahawa hiyo inatoka nchini Kenya katika Nyeri County ambapo Muthoni alizaliwa na kulia. Muthoni ni mwanamke ambaye kwa hali ya juu amekuwa mstari wa mbele kwenye kujali hali ya wakulima, bei za uzaji na maisha ya wafanyakazi wa mashamba kwa ujumla.

Mwaka 2012 nilipata nafasi ya kuionja ladha ya kahawa hiyo na baada ya sipu moja tu nikawa mpenzi wa kahawa hiyo namba moja!

 

Kahawa nzuri kwangu mimi ni kahawa yenye ladha nzuri, maridhawa, na yenye kujali wazalishaji na waandalizi wote hususani wakulima.

 

 

Asanteni sana kwa ushirikiano wenu mbubwa mno kwa kuwaimarisha wakulima wa kahawa hususan wa nchi ya Kenya na Afrika Mashariki!

Mungu awabariki sana.

 

Kwa kununua bidhaa zetu, bonyeza hapa